Biashara ya zero spread kwenye Deriv MT5 | Deriv Blog

Fanya biashara kwa usahihi kwenye Deriv MT5 kwa biashara ya zero spread. Tekeleza biashara karibu na bei ya soko bila spread na kamisheni zisizobadilika.

Timu ya Deriv · 26 June 2024 · 3 dak kusoma

Share

Deriv inayo furaha kutambulisha akaunti ya zero spread, ambayo sasa inapatikana kwenye jukwaa lenye nguvu la Deriv MT5. Fanya biashara ya rasilimali zako za kifedha unazozipenda na Fahirisi za Synthetic na ujionee kiwango kipya cha uwazi na unafuu wa gharama.

Zero spread inamaanisha nini kwako?

Biashara ya zero spread inamaanisha kuwa hakuna tofauti kati ya bei za kununua (ask) na kuuza (bid) za rasilimali. Kwa kuwa hakuna spread ya kuzingatiwa, biashara zako zinatekelezwa karibu zaidi na bei ya soko, na kukupa udhibiti mkubwa zaidi wa maeneo yako ya kuingia na kutoka kwenye soko. Hiyo inamaanisha unaweza:

  • Kupata bei unayotaka: Ukiwa na zero spread, unanunua au kuuza kwa bei iliyo karibu iwezekanavyo na bei ya soko, siyo kwa bei mbaya kidogo kutokana na spread.
  • Kuingia na kutoka kwenye biashara kwa haraka zaidi: Kwa sababu hakuna spread ya kusubiri, biashara zako zinaweza kutekelezwa papo hapo kwa bei ya soko, na hivyo kuruhusu kuchukua hatua za haraka kulingana na mabadiliko ya bei.

Hili linafaidisha hasa wafanyabiashara wa mara kwa mara, scalpers, na wale wanaotumia mikakati ya biashara inayojiendesha yenyewe.

Deriv MT5: Kitovu chako cha biashara ya zero spread

Ingia kwenye biashara ya zero spread ukitumia Deriv MT5. Jukwaa letu la kisasa linatoa uzoefu mzuri na rahisi unaokuja na zana unazohitaji ili kuchambua masoko, kutekeleza biashara, na kudhibiti hatari kwa ufanisi.

​Deriv MT5 inatoa anuwai kubwa ya zana za synthetic na za kifedha kwa ajili ya biashara ya zero spread. Ukiwa na uwezo wa kufikia pea kubwa na ndogo za forex, bidhaa, fahirisi za hisa, na mengine mengi, unaweza kuongeza uwezekano wako wa kufanya biashara ukitumia Leverage ya hadi 1:1000. Hapa kuna orodha ya rasilimali zote zinazopatikana ili kufanya biashara ukitumia akaunti yako ya zero spread.

Vyovyote vile mapendeleo yako ya biashara yalivyo, utapata fursa za kutosha kwenye Deriv MT5.

Kwa nini uchague Deriv kwa biashara ya zero spread?

  • Kupunguza gharama za biashara: Ondoa gharama za spread na uweze kuongeza faida yako.
  • Upangaji bei ulio wazi: Pata ufikiaji wa moja kwa moja wa bei za soko kwa utekelezaji sahihi wa biashara.
  • Kamisheni zisizobadilika, si spreads: Furahia gharama za biashara zinazotabirika ukiwa na kamisheni zisizobadilika, bila kujali mabadiliko ya haraka ya soko.
  • Hakuna kuongezeka kwa spread wakati wa mabadiliko ya haraka: Fanya biashara kwa ujasiri, ukijua kuwa gharama zako hazitaongezeka bila kutarajia wakati wa hali ya soko inayobadilika haraka.

Kubali mustakabali wa biashara ukitumia akaunti ya zero spread ya Deriv. Jionee upangaji bei ulio wazi, gharama zinazotabirika, na uzoefu rahisi wa kufanya biashara kwenye Deriv MT5. Fungua akaunti yako ya zero spread leo na uchunguze fursa zote zinazokusubiri.

Kumbuka: Biashara inahusisha hatari, na akaunti ya zero spread haifai kwa wafanyabiashara wote. Kuunda mkakati madhubuti wa biashara ni muhimu sana kabla ya kujihusisha na biashara ya zero spread.

Join 3M+ global traders

Open an account in minutes and start trading the world's markets — forex, stocks, indices, and more.