Kwa Nini Hisa Mpya Sokoni Kama Vile SpaceX Hupanda na Kushuka kwa Kasi Mwanzoni?
Bei ya SpaceX inapangwa na wastani wa asilimia 3 hadi 5 ya hisa zinazoweza kufanyiwa biashara (tradable float). Hii hapa ni sababu inayoifanya idadi ndogo ya hisa kusababisha mabadiliko makubwa ya bei za IPO na jinsi ya kuyaelewa.
Timu ya Deriv · 24 June 2026 · 4 dak kusoma

Bei ya hisa inapangwa tu na hisa zinazoweza kufanyiwa biashara kwa uhalisia. Sehemu hiyo inapokuwa ndogo, bei hupanda na kushuka kwa kasi sana na inakupa picha kuhusu uhaba wa hisa, badala ya thamani ya kampuni.
SpaceX (SPCX) iliingia sokoni mnamo 12 Juni 2026 kwa bei ya USD 135. Ndani ya siku chache ilipanda hadi kufikia kiwango cha juu zaidi kuwahi kutokea cha takriban USD 226, kisha ikashuka hadi karibu na USD 150. Biashara haikubadilika sana katika muda wa wiki mbili. Mabadiliko hayo yalichangiwa na kiwango cha hisa zinazopatikana (float).

Je, "thin float" inamaanisha nini, na kwa nini ni muhimu?
Float ni sehemu ya hisa zinazoweza kufanyiwa biashara kwa uhuru. Kwa upande wa SpaceX, inakadiriwa kuwa asilimia 3 hadi 5 ya hisa zake ndizo zinazoweza kufanyiwa biashara kiuhalisia. Zilizosalia zimezuiliwa kwa wafanyakazi wa ndani na wawekezaji wa awali.
Kwa hivyo, bei inayofuatiliwa na mamilioni ya watu inapangwa na sehemu ndogo sana ya kampuni. Uchache wa hisa zinazopatikana (small float) inamaanisha idadi ndogo ya wanunuzi na wauzaji ndiyo wanaopanga bei kwa ajili ya kila mtu. Wakati mahitaji yanapozidi kiwango hicho kidogo cha usambazaji, bei hupanda kwa haraka sana. Msisimko huo unapoisha, bei hushuka kwa haraka vilevile.
Kwa nini ongezeko kubwa la mahitaji huathiri sana uchache wa hisa (small float)
Fikiria uwanja wa michezo wenye lango moja tu la kutokea lililo wazi. Wakati kila mtu anapotaka kuingia, lango hilo huonekana kuwa la thamani sana. Kundi la watu linapoamua kutoka, mlango huo mwembamba hufanya kutoka kuwa vigumu sana.
Hivyo ndivyo ilivyo kwa hisa za 'thin-float'. Udogo huo hukuza hisia zozote za watu. Uhaba hukuza mienendo ya bei katika pande zote mbili, ikipanda wakati wa kuingia na kushuka wakati wa kutoka. Kampuni kubwa iliyokomaa sokoni kama vile Amazon hufanya biashara ya mabilioni ya dola za usambazaji halisi kila siku, hivyo basi biashara moja haiwezi kusababisha mabadiliko makubwa. IPO mpya iliyo na kiwango kikubwa cha hisa kilichozuiliwa (locked-up float) haina ulinzi kama huo.
Je, jambo hili limewahi kutokea hapo awali?
Mara kwa mara. Mnamo mwaka 2011, LinkedIn ilitoa asilimia 8 pekee ya hisa zake kwa umma na ikapanda kwa zaidi ya asilimia 80 katika siku ya kwanza, kisha iliendelea kubadilika kwa kasi kwa miezi kadhaa hadi usambazaji zaidi ulipoingia sokoni. Saudi Aramco ilitoa karibu asilimia 1.5 ya hisa zake kwa umma mnamo 2019, na kiasi hicho kidogo kilipandisha thamani ya hisa hali iliyozua mashaka ya muda mrefu.
Rivian inatumika kama onyo. Ilitoa kiasi kidogo tu cha hisa mnamo 2021, na kwa muda mfupi ilizidi thamani ya watengenezaji maarufu wa magari, kisha ikashuka kwa zaidi ya asilimia 80 kutoka kiwango chake cha juu zaidi wakati vipindi vya kuzuia uuzaji (lock-ups) vilipoisha na hisa halisi kuingia sokoni. Msisimko wa hisa chache sokoni (thin-float) mara nyingi hubadilika pindi usambazaji halisi unapoingia sokoni.
Unapaswa kuielewa vipi bei ya SpaceX kwa sasa?
Kwa uangalifu, huku ukizingatia kiwango cha hisa zinazopatikana. Kushuka kwa bei hadi kufikia karibu USD 150 hakumaanishi moja kwa moja kwamba biashara imeshuka thamani. Uhaba unaweza pia kukuza anguko, kwa hivyo sehemu ya anguko hilo inaweza kuwa inasababishwa na uhaba uleule wa hisa unaofanya kazi kinyume chake.
Tofauti ya makadirio ya thamani inathibitisha yote. Morningstar inaweka thamani halisi kuwa karibu USD 63. Wastani wa wachambuzi watano wa Wall Street unaonyesha kuwa juu ya USD 235. Wakati wachambuzi wakuu wanapotofautiana kwa kiasi hicho, inamaanisha kiwango cha hisa zilizopo sokoni (float) kinaleta athari kubwa zaidi kuliko taarifa za msingi za kampuni (fundamentals). Uongozi wa SpaceX katika kurusha roketi angani na mapato ya Starlink ni halisi, lakini mwenendo wa bei una mabadiliko mengi kimakusudi kutokana na muundo wa hisa hizo.
Dalili muhimu ya kufuatilia ni pale hisa nyingi zaidi zitakaporuhusiwa kuingia sokoni. Kipindi cha kuzuia uuzaji kinapoisha, usambazaji huongezeka na ongezeko la thamani kutokana na uhaba (scarcity premium) linaweza kushuka haraka. Iwapo bei itaanza kufuata mafanikio ya kampuni badala ya mabadiliko yanayoendeshwa na kiwango cha hisa, hiyo ni dalili kwamba uundaji wa bei halisi unaimarika. Bidhaa za leverage kama vile 2X SpaceX ETF hukuza kila moja ya mabadiliko haya, pamoja na kushuka kwa thamani kwa kurejeshwa upya (daily-reset decay) katika masoko yenye mabadiliko ya haraka, kwa hivyo hukuza zaidi "kelele" za soko badala ya kuzifanya zieleweke.
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
Kipindi cha kuzuia uuzaji (lock-up) ni muda maalum, mara nyingi kuanzia siku 90 hadi 180, ambapo wafanyakazi wa ndani na wawekezaji wa awali huzuiwa kuuza hisa zao. Muda huo unapoisha, hisa zaidi zinaweza kufanyiwa biashara, na hivyo kuongeza usambazaji na mara nyingi kupunguza ongezeko la bei lililosababishwa na uhaba.
Tofauti kubwa iliyopo, kuanzia thamani halisi ya takriban USD 63 ya Morningstar hadi wastani wa zaidi ya USD 235 wa Wall Street, inaonyesha sintofahamu kubwa kuhusu hisa mpya sokoni inayoingia ikiwa na kiasi kidogo sana cha hisa (thin float). Tofauti hii yenyewe inaonyesha kuwa kiwango cha hisa zinazopatikana (float) kinaendesha mabadiliko ya bei zaidi kuliko taarifa za msingi za kampuni.
Ndiyo. ETF ya mara 2 ya kila siku (2X daily ETF) hulenga kupata takriban mara mbili ya mabadiliko ya kila siku ya hisa na hujirejesha upya kila siku (resets daily), jambo ambalo husababisha kushuka kwa thamani katika masoko yenye mabadiliko ya haraka na yasiyotabirika. Katika hisa yenye mabadiliko ya mara kwa mara kutokana na uhaba wa hisa sokoni, hii hukuza mabadiliko ya kushuka na kupanda pamoja na anguko.
Sio lazima. Ukiwa na hisa chache sokoni, uhaba unaweza kukuza kushuka na hata kupanda kwa bei, hivyo kushuka kunaweza kuwa kunasababishwa na uhaba wa hisa badala ya maamuzi kuhusu biashara yenyewe. Fuatilia ili kuona kama bei inaanza kufuata mafanikio halisi ya kampuni.