Vipengele 4 kwa ajili ya usimamizi bora wa hatari kwenye Multipliers za Deriv | Deriv Blog

Gundua zana unazoweza kutumia kwa usimamizi bora wa hatari katika biashara unapofanya biashara kwa kutumia Multipliers za Deriv.

Timu ya Deriv · 21 July 2022 · 3 dak kusoma

Share

Makala haya yalisasishwa tarehe 22 Januari 2024

Kufanya biashara na Multipliers ni njia nzuri ya kuongeza faida yako inayowezekana. Kwenye majukwaa ya biashara ya Deriv, unaweza pia kuepuka hasara kubwa wakati soko linapokwenda kinyume nawe. Katika chapisho hili la blogu, tunaeleza jinsi vipengele vya usimamizi wa hatari kwenye majukwaa ya Deriv vinavyoyafanya kuwa chaguo bora kwa biashara ya Multipliers.

Njia 4 ambazo Deriv inakupa udhibiti zaidi kwenye biashara yako ya Multipliers 

Stop Out ya kiotomatiki 

Unapofanya biashara kwa kutumia Multipliers kwenye Deriv, huwezi kamwe kupoteza zaidi ya kiasi chako cha biashara. Ukiwa na kipengele cha Stop Out ya kiotomatiki, nafasi zako zitafungwa moja kwa moja pindi hasara yako inapolingana na kiasi chako cha biashara. 

Take Profit

Kwa kawaida, utahitaji kufunga nafasi yako mwenyewe ili kupata faida yako. 

Kipengele cha Take Profit hukuruhusu kufanya mchakato huu uwe wa kiotomatiki. Unachotakiwa kufanya ni kuweka kiwango cha faida ambacho utaridhika nacho. Ikiwa faida yako itafikia au kuzidi kiasi hiki, nafasi yako itafungwa na faida yako itaongezwa kwenye salio lako la akaunti. 

Stop Loss

Stop Loss inakuwezesha kuweka kiasi halisi ambacho uko tayari kukihatarisha. Unaweza kupunguza hasara yako kabla ya kupoteza kiasi chako chote cha biashara. 

Kila mara hasara yako inapolingana au kuzidi kiasi chako cha Stop Loss, biashara yako itafungwa moja kwa moja. 

Kwa mfano, unafungua biashara na kiasi cha biashara cha USD 10. Stop Out ya kiotomatiki itafunga biashara yako hasara yako inapofikia USD 10. Hata hivyo, ikiwa unataka kupunguza hasara zaidi, unaweza kuweka kiwango cha Stop Loss cha USD 5. Hasara yako inapofikia kiasi hiki, biashara yako itafungwa kiotomatiki.

Kughairi muamala

Umefungua biashara, lakini umeanza kuwa na shaka? Ukiwa na kipengele cha kughairi muamala, una chaguo la kughairi biashara ndani ya muda uliochaguliwa (kulingana na soko na rasilimali unayofanyia biashara) baada ya kuifungua na kurudisha kiasi chako cha biashara. Tafadhali kumbuka kuwa Deriv inatoza ada ndogo kwa huduma hii.

---

Ukiwa na vipengele hivi 4 vya usimamizi wa hatari, kufanya biashara ya Multipliers kwenye Deriv kunaweza kukusaidia kuepuka kukosa fursa na kukuzuia kupoteza zaidi ya unachotaka kupoteza. Ingia au jisajili kwa ajili ya akaunti ya onyesho ya bure ili ujaribu Multipliers za Deriv. 

Join 3M+ global traders

Open an account in minutes and start trading the world's markets — forex, stocks, indices, and more.