Kuchunguza mkakati wa Oscar's Grind kwenye Deriv Bot | Deriv Blog

Chunguza Oscar's Grind, mkakati wenye hatari ndogo, na jinsi ya kuutumia kwenye Deriv Bot kwa biashara ya kiotomatiki, pamoja na udhibiti madhubuti wa hatari.

Timu ya Deriv · 7 November 2023 · 3 dak kusoma

Share

Makala haya yalisasishwa tarehe 17 Januari 2024

Mkakati wa Oscar's Grind umeundwa ili kupata faida ya kiasi lakini thabiti katika kila kipindi cha biashara. Mkakati huu unagawa biashara katika vipindi na una kanuni tatu.

Vigezo vya biashara

  • Kiasi cha awali cha biashara: Kiasi unacholipa ili kuanza biashara.
  • Kikomo cha faida: Bot itaacha kufanya biashara ikiwa jumla ya faida yako itazidi kiasi hiki.
  • Kikomo cha hasara: Bot itaacha kufanya biashara ikiwa jumla ya hasara yako itazidi kiasi hiki.
Chati inayoonyesha mkakati wa Oscar's Grind kwenye Deriv Bot

Kanuni ya 1: Mkakati unalenga uwezekano wa kupata kizio kimoja cha faida kwa kila kipindi

Jedwali hapo juu linaonyesha kanuni hii kwa kuonyesha kwamba pindi biashara yenye mafanikio inapotokea na kufikia lengo la kizio kimoja cha faida inayotarajiwa, ambayo ni USD 1 katika mfano huu, kipindi hicho kinakamilika. Ikiwa biashara itaendelea, kipindi kipya kitaanza.

Kanuni ya 2: Kiasi cha biashara huongezeka tu wakati biashara iliyopata hasara inafuatiwa na biashara iliyofanikiwa

Jedwali linaonyesha kanuni hii katika kipindi cha pili. Baada ya biashara kuleta hasara katika mzunguko wa 4, na kufuatiwa na biashara yenye mafanikio katika mzunguko wa 5, kiasi cha biashara kitaongezeka hadi USD 2 kwa mzunguko wa 6. Hii inaendana na sheria ya mkakati ya kuongeza kiasi cha biashara tu baada ya hasara kufuatiwa na biashara iliyofanikiwa.

Kanuni ya 3: Kiasi cha biashara hurekebishwa kulingana na ukubwa wa tofauti kati ya hasara ya sasa na faida inayolengwa kwa kipindi.

Katika mzunguko wa 7, kiasi cha biashara kinapunguzwa kutoka USD 2 hadi USD 1, ili kufikia faida inayolengwa ya USD 1.

Marekebisho ya kiasi cha biashara: faida inayolengwa ya kipindi (USD 1) - faida ya sasa ya kipindi (USD 0) = USD 1

Kipindi cha pili kinakamilika baada ya kufikia lengo la kizio kimoja cha faida inayotarajiwa kwa kila kipindi, sawa na USD 1. Ikiwa biashara itaendelea, kipindi kipya kitaanza tena. 

Viwango vya kikomo cha faida na hasara

Kwa kutumia Deriv Bot, wafanyabiashara wanaweza kuweka viwango vya kikomo cha faida na hasara ili kulinda faida zinazoweza kupatikana na kupunguza uwezekano wa hasara. Hii inamaanisha bot ya biashara itasimama kiotomatiki wakati kikomo cha faida au hasara kitakapofikiwa. Aina hii ya udhibiti wa hatari inaweza kuongeza nafasi za biashara zilizofanikiwa huku ikipunguza athari za hasara. Kwa mfano, ikiwa mfanyabiashara ataweka kikomo cha faida kuwa USD 100 na mkakati ukazidi USD 100 za faida kutoka kwa biashara zote, basi bot itasimama kufanya kazi.

Muhtasari

Mkakati wa Oscar's Grind unatoa mbinu yenye nidhamu ya kupata faida kidogokidogo kupitia ongezeko la kimfumo la kiasi cha biashara. Inapounganishwa kwenye Deriv Bot na udhibiti mzuri wa hatari, kama vile viwango vya kikomo cha faida au hasara, huwapa wafanyabiashara mbinu yenye nguvu ya biashara ya kiotomatiki. Hata hivyo, wafanyabiashara wanapaswa kutathmini kwa kina uvumilivu wao wa hatari na kujaribu kufanya biashara kwenye akaunti ya onyesho (demo) ili kuzoea mkakati kabla ya kufanya biashara kwa pesa halisi.

Join 3M+ global traders

Open an account in minutes and start trading the world's markets — forex, stocks, indices, and more.