Jinsi ya kutambua na kuripoti utapeli wa phishing | Deriv Blog

Jifunze hatua muhimu za kutambua na kuripoti utapeli wa phishing. Linda data na fedha zako mtandaoni kwa mwongozo wetu wa jinsi ya kutambua na kukabiliana na vitisho vya phishing.

Timu ya Deriv · 3 October 2023 · 8 dak kusoma

Share

Fikiria unaperuzi ukurasa wako wa Instagram na ghafla unapata ujumbe kwenye DM yako. Umetoka kwa akaunti ambayo huifuatilii, na inaonekana kuendeshwa na mabalozi wa chapa wa kampuni unayoipenda zaidi. Katika ujumbe wao, wanaahidi kukutumia baadhi ya bidhaa bure ikiwa utabofya kiungo (link) kilichoambatishwa.

Je, utabofya kiungo hicho au la?

Katika enzi hii ya kidijitali, kulinda utambulisho na akaunti zako mtandaoni ni muhimu sana kwa kuwa matapeli wanazidi kuwa wajanja kwa majaribio yao ya phishing.

Phishing ni shambulio la kimtandao ambapo matapeli hujaribu kukuhadaa ili utoe taarifa nyeti kama vile nywila (passwords) na maelezo ya benki yako. Wao hujifanya kama kampuni halisi na kutengeneza barua pepe bandia, wasifu wa mitandao ya kijamii, na namba za simu ili kukushawishi uchukue hatua zinazohatarisha usalama wako. Kosa moja la kubofya linaweza kuweka data zako wazi kwa matapeli.

Endelea kusoma ili kujifunza jinsi ya kutambua na kuripoti utapeli wa phishing ili kuimarisha usalama wako mtandaoni.

Barua pepe

Kutambua barua pepe za phishing kunaweza kuwa kugumu. Kuwa mwangalifu na dalili hizi za onyo za barua pepe ya kitapeli:

mfano wa barua pepe ya phishing kutoka kwenye barua pepe ya deriv

Dalili za kawaida za hatari kwenye barua pepe ya phishing:

  • Anwani ngeni ya barua pepe ya mtumaji. Deriv hutuma barua pepe zikiwa na anwani inayoishia na @deriv.com.
  • Makosa ya tahajia na sarufi.
  • Wanakuomba ubofye viungo na viambatisho vinavyotia shaka.
  • Ahadi za kupata pesa kwa urahisi na faida kubwa.
  • Maombi ya kuchukua hatua za haraka kama vile kuhamisha pesa zako kwenda kwenye akaunti ya benki.

Dalili zisizo za kawaida za hatari kwenye barua pepe ya phishing:

  • Lugha yenye heshima au rasmi kupita kiasi: Barua pepe za phishing wakati mwingine hutumia lugha ya heshima au rasmi kupita kiasi ili kujenga hisia za uongo za weledi na uaminifu.
  • Maombi yasiyo ya kawaida ya taarifa: Barua pepe za kitapeli zinaweza kuomba taarifa zisizo za kawaida, kama vile jina la utotoni la mama yako, jina la mnyama wako wa kipenzi wa utotoni, au jina la mji uliolelewa. Haya ni maswali ya kawaida ya kiusalama ambayo, kama tapeli ana majibu yake, yanaweza kutumika kuweka upya nywila yako na kufikia akaunti yako.
  • Mabadiliko ya ghafla ya saini ya barua pepe: Ukigundua mabadiliko ya ghafla kwenye saini ya barua pepe ya mtumaji, kama vile jina tofauti au maelezo ya mawasiliano, hii inawezekana kabisa kuwa ni barua pepe ya phishing.
  • URL zilizofupishwa: Matapeli mara nyingi hutumia huduma za kufupisha URL ili kuficha viungo hatari. URL hufupishwa ili kiungo kisionyeshe tovuti halisi ukiweka kishale chako (cursor) juu yake.

Ukipokea barua pepe kutoka kwa mtu anayejifanya kutoka Deriv, tafadhali turipoti kupitia live chat. Wasiliana nasi ikiwa una wasiwasi, na tutathibitisha kama tunahitaji chochote kutoka kwako.

Akaunti za mitandao ya kijamii

Sasa inapokuja kwenye wasifu bandia wa mitandao ya kijamii, lazima tuwe waangalifu zaidi mtandaoni. Kuwa mwangalifu na dalili hizi za onyo ili kuhakikisha hutokuwa mwathirika mwingine wa utapeli:

__wf_reserved_inherit

Dalili za kawaida za hatari kwenye wasifu bandia wa mitandao ya kijamii:

  • Makosa ya mara kwa mara ya tahajia na sarufi.
  • Kukosewa kwa tahajia ya jina la akaunti.
  • Uwiano mkubwa kati ya idadi ya watu anaowafuata na wale wanaomfuata.
  • Ofa zilizojaa emoji zinazosikika kuwa nzuri kupita kiasi.
  • Marafiki/wafuasi wachache au hakuna kabisa.

Dalili zisizo za kawaida za hatari kwenye wasifu bandia wa mtandao wa kijamii:

  • Machapisho mengi sana kwa muda mfupi: Akaunti za kitapeli zinaweza kuchapisha picha au hadithi (stories) nyingi kwa muda mfupi ili kupata tahadhari na wafuasi haraka.
  • Kutangaza bidhaa bandia: Matapeli mara nyingi hutangaza bidhaa bandia au za kubahatisha, ambazo hazihusiani na kampuni husika.
  • Maombi ya ajabu ya urafiki/kufuata: Matapeli mara nyingi hutengeneza wasifu bandia na kukutumia maombi ya urafiki/kufuata. Akaunti hizi kwa kawaida huwa na marafiki wachache, taarifa binafsi chache sana, na hakuna marafiki wa pamoja (mutual connections).
  • Maombi ya malipo: Matapeli wanaweza kukuomba ufanye malipo au kuhamisha pesa nje ya jukwaa letu. Tafadhali kumbuka kwamba ikiwa Deriv inahitaji taarifa yoyote binafsi, ombi litatumwa kupitia barua pepe yetu rasmi au live chat.
__wf_reserved_inherit

Ikiwa utakutana na akaunti bandia ya mtandao wa kijamii, gusa nukta 3 kwenye wasifu kisha bofya Ripoti (Report) ili kuiripoti akaunti hiyo kama ya kitapeli. Utaratibu huu utachukua chini ya dakika moja na kuusaidia mtandao kuchukua hatua stahiki.

Baada ya kuripoti wasifu huo bandia, tafadhali toa picha za skrini (screenshots) za akaunti yao kwa timu yetu ya Huduma kwa Wateja kupitia live chat ili tuweze kuchukua hatua za ziada.

Programu ya kutuma ujumbe

Mbali na wasifu bandia wa mitandao ya kijamii, matapeli pia hutengeneza akaunti bandia za kutuma ujumbe kwenye WhatsApp ili kumlenga mtumiaji moja kwa moja. Hakikisha unaangalia dalili hizi za akaunti ya kitapeli ya kutuma ujumbe na kufahamu jinsi ya kuziripoti kwa ufanisi.

Mfano wa jumbe za utapeli za WhatsApp kutoka kwenye namba bandia ya Deriv

Dalili za kawaida za hatari kwenye akaunti ya kitapeli ya kutuma ujumbe:

  • Makosa ya tahajia na sarufi kwenye ujumbe.
  • Maelekezo ya kubofya viungo au kupakua programu.
  • Ahadi za faida kubwa na pesa za haraka.
  • Maombi ya haraka ya data binafsi kama vile nywila yako na maelezo ya benki.

Dalili zisizo za kawaida za hatari kwenye akaunti ya kitapeli ya kutuma ujumbe:

  • Matumizi makubwa ya bot: Matapeli wanaweza kutumia bot kuwasiliana nawe kwa jumbe zinazojiendesha (automated messages) au viungo vya tovuti za kitapeli. Ikiwa mazungumzo yanaonekana yamepangiliwa sana au si ya asili, inaweza kuwa ni utapeli.
  • Huduma kwa wateja bandia: Baadhi ya matapeli hujifanya kuwa mawakala wa huduma kwa wateja na kutoa msaada kwenye masuala ambayo hukuomba msaada kwayo.
  • Jumbe za kutiliwa shaka zinazosambazwa (forwarded): Ikiwa mtu usiyemfahamu vizuri atakusambazia jumbe au faili bila muktadha (context) wowote, inaweza kuwa ni jaribio la kusambaza utapeli au virusi.
  • Kujifanya kama watu unaowaamini: Matapeli wanaweza kujifanya kama watu unaowaamini kwa kutumia picha za wasifu na majina ya watumiaji (usernames) yanayofanana.

Ukikutana na wasifu bandia kwenye programu ya kutuma ujumbe, gusa kwenye wasifu wa akaunti kisha bofya Ripoti (Report) ili kuiripoti akaunti hiyo kama ya kitapeli. Utaratibu huu utachukua chini ya dakika moja na kuusaidia mtandao husika kuchukua hatua stahiki.

Baada ya kuripoti wasifu huo bandia, tafadhali toa picha za skrini za akaunti yao kwa timu yetu ya Huduma kwa Wateja kupitia live chat ili tuweze kuchukua hatua za ziada.

Mbinu bora za kuepuka phishing kwa ujumla

Kwa kuwa sasa unaweza kutambua na kuchukua hatua dhidi ya majaribio ya phishing, sikuzote kumbuka Mambo 5 Usiyopaswa Kufanya unapotumia barua pepe na akaunti za mtandaoni:

  1. Usibofye viungo au kupakua faili mara moja.
  2. Usishiriki taarifa zako binafsi.
  3. Usichukue hatua mara moja ikiwa unashinikizwa kufanya hivyo.
  4. Usiogope kuwasiliana na timu yetu ya Huduma kwa Wateja kupitia live chat ukiwa na shaka au wasiwasi.
  5. Usijibu barua pepe, simu, na jumbe zinazotia shaka.

Endelea kuwasiliana nasi kwa taarifa mpya kwenye akaunti zetu za kimataifa:

Kwa taarifa mahususi za EU (Umoja wa Ulaya):

Unahitaji msaada? Wasiliana na huduma yetu ya msaada kupitia WhatsApp: +356 9957 8341.

Kwa vidokezo zaidi vya usalama, soma chapisho la blogu yetu la Jinsi ya kulinda akaunti yako ya biashara mtandaoni au chapisho la Jinsi ya kuepuka utapeli katika biashara.

Join 3M+ global traders

Open an account in minutes and start trading the world's markets — forex, stocks, indices, and more.