Kuchunguza mkakati wa D'Alembert kwenye Deriv Bot | Deriv Blog
Gundua jinsi ya kutekeleza mkakati wa D'Alembert na vidokezo muhimu vya mafanikio unapoitumia pamoja na vipengele vya biashara vya kiotomatiki vya Deriv Bot.
Timu ya Deriv · 6 November 2023 · 4 dak kusoma

Makala haya yalisasishwa tarehe 17 Januari 2024
Mkakati wa D'Alembert unahusisha kuongeza kiasi chako cha biashara baada ya kupata hasara na kukipunguza baada ya kupata faida kwenye biashara kwa idadi ya uniti iliyopangwa tayari.
Hivi ndivyo vigezo vya biashara vinavyotumika kwenye mkakati wa D'Alembert katika Deriv Bot.
Kiasi cha kuanzia cha biashara: Kiasi unacholipa ili kuingia kwenye biashara. Kiasi ambacho uko tayari kukiweka kama kiasi cha biashara ili kuingia kwenye biashara. Katika mfano huu, tutatumia USD 1.
Uniti: Idadi ya uniti zinazoongezwa ikiwa biashara inaleta hasara au idadi ya uniti zinazoondolewa ikiwa biashara inaleta faida. Kwa mfano, ikiwa uniti imewekwa kuwa 2, kiasi cha biashara huongezeka au kupungua mara mbili ya kiasi cha kuanzia cha USD 1, ikimaanisha kinabadilika kwa USD 2.
Kikomo cha faida: Bot itaacha kufanya biashara ikiwa jumla ya faida yako itazidi kiasi hiki.
Kikomo cha hasara: Bot itaacha kufanya biashara ikiwa jumla ya hasara yako itazidi kiasi hiki.
Mfano wa Mkakati wa D'Alembert

- Anza na kiasi cha kuanzia cha biashara. Katika mfano huu, tutatumia USD 1.
- Weka uniti unayopendelea. Katika mfano huu, ni uniti 2 au USD 2.
- Ikiwa biashara ya kwanza italeta faida, kiasi cha biashara kwa biashara inayofuata hakitapungua bali kitabaki kwenye kiasi cha kuanzia. Mkakati huu unafanya biashara kwa kiwango cha chini kabisa cha USD 1. Angalia A1.
- Ikiwa biashara ya pili italeta hasara, Deriv Bot itaongeza kiasi chako cha biashara kiotomatiki kwa biashara inayofuata kwa USD 2. Deriv Bot itaendelea kuongeza USD 2 kwenye kiasi cha biashara cha mzunguko uliopita baada ya kila biashara inayopata hasara. Angalia A2.
- Ikiwa biashara zinazofuata zinaleta faida, kiasi cha biashara kwa biashara inayofuata kitapunguzwa kwa USD 2. Hii inaweza kuonyeshwa hapo juu ambapo kiasi cha biashara cha USD 3 kinapunguzwa hadi USD 1. Angalia A3.
Vikomo vya faida na hasara
Wakiwa na Deriv Bot, wafanyabiashara wanaweza kuweka vikomo vya faida na hasara ili kulinda faida zinazowezekana na kudhibiti hasara zinazoweza kutokea. Hii inamaanisha kuwa bot ya biashara itasimama kiotomatiki wakati kikomo cha faida au hasara kitakapofikiwa. Ni aina ya usimamizi wa hatari inayoweza kuongeza mapato. Kwa mfano, ikiwa mfanyabiashara ataweka kikomo cha faida kuwa USD 100 na mkakati ukazidi USD 100 za faida kutokana na biashara zote, basi bot itaacha kufanya kazi.
Kukokotoa hatari yako
Mkakati wa D'Alembert una hatari ndogo ukilinganisha na Martingale, lakini bado unaweza kutathmini jinsi fedha zako zitakavyodumu kwa mkakati huu kabla ya kufanya biashara. Tumia fomula hii kwa urahisi.
B = Kikomo cha hasara
s = kiasi cha kuanzia cha biashara
R = idadi ya mizunguko
f = ongezeko la uniti

Kwa mfano, ikiwa una kikomo cha hasara (B) cha USD 100, kikiwa na kiasi cha kuanzia cha biashara (s) cha USD 1 na ongezeko la uniti 2 (f), mkokotoo utakuwa hivi:

Hii inamaanisha baada ya mizunguko 10 ya hasara mfululizo, mfanyabiashara atapoteza USD 100. Hii inafikia kikomo cha hasara cha USD 100, na kuisimamisha bot.
Muhtasari
Mfumo wa D'Alembert unatoa uwiano mzuri zaidi wa kufanya biashara kupitia ongezeko lililodhibitiwa la kiasi cha biashara. Ukiwa na usimamizi madhubuti wa hatari kama vile vikomo vya kiasi cha biashara, unaweza kujiendesha vyema kwenye Deriv Bot. Hata hivyo, wafanyabiashara wanapaswa kutathmini kikamilifu kiwango chao cha kuhimili hatari, kujaribu mikakati kwenye akaunti ya demo ili iendane na mtindo wao wa biashara kabla ya kufanya biashara na pesa halisi. Hii inaruhusu kuboresha mbinu na kuweka uwiano kati ya faida na hasara zinazoweza kupatikana wakati wa kudhibiti hatari.