Epuka makosa ya kawaida ya ufanyaji biashara kwa hatua hizi 4 | Deriv Blog
Makosa ya kawaida ya ufanyaji biashara yanaweza kuepukwa kwa hatua hizi 4. Tembelea blogu yetu ili ujifunze zaidi.
Timu ya Deriv · 8 September 2022 · 5 dak kusoma

Wafanyabiashara wanaoanza mara nyingi huona ufanyaji biashara kuwa wa kutisha na huhofia kufanya makosa. Lakini je, ulijua kuwa makosa ya kawaida ya ufanyaji biashara hayawahusu wanaoanza pekee? Hata wafanyabiashara wazoefu hufanya makosa. Suluhisho la kuyaepuka lipo katika kuunda mbinu iliyopangwa na yenye nidhamu katika ufanyaji biashara, na blogu hii inaeleza jinsi ya kufanya hivyo kwa hatua 4.
Baadhi ya makosa ya kawaida ambayo wafanyabiashara hufanya ni…

…orodha inaweza kuendelea. Sasa, masoko ya kifedha hayatabiriki, lakini unaweza kujaribu kuepuka makosa haya (na mengine kadhaa) ya ufanyaji biashara kwa kufuata mpango huu wa utekelezaji wa hatua 4. Hatua hizi si kamilifu kwa asilimia mia moja lakini ni njia nzuri ya kukusaidia kujenga tabia ya kufanya maamuzi ya kibiashara yanayowajibika zaidi.
Hatua 1 – Kupanga ni biashara zipi za kuanza na wakati gani
Kinyume na wanavyofikiri watu wengi, kufanya biashara yenye uwezekano wa kufanikiwa hakuhusiani sana na bahati bali kunahusiana zaidi na kupanga biashara zako kwa njia yenye nidhamu. Utabiri wako unahitaji kufikiriwa kwa kina na kutegemea utafiti wa ukweli unaojumuisha tathmini ya hali ya soko.
Andaa mpango wa biashara unaojumuisha kuchambua matukio ya sasa ya kimataifa na kiuchumi na ufanye utafiti wako kuhusu jinsi masoko yanavyoitikia matukio hayo. Ikiwa una muda mchache wa utafiti na uchambuzi, tumia mtaji mdogo kufanya biashara kwenye soko 1 au yasiyozidi 2 kwa wakati mmoja. Mpango huu wa biashara utakusaidia kuchambua fursa za biashara kwa vitendo na kwa lengo thabiti huku pia ukigundua ni rasilimali ipi inayofaa zaidi kwa kiwango chako cha kukabiliana na hatari.
Hatua 2 – Kupanga ni biashara zipi za kufunga na wakati gani
Kila mfanyabiashara hufikiria wakati wa kuanza biashara. Ni wachache sana wanaojua jinsi ya kuchambua wakati wa kuifunga. Wafanyabiashara huishia kupata hasara zaidi kwenye biashara zinazopoteza kwa matumaini kwamba soko litabadilika na hasara itageuka kuwa faida. Mpango wa mkakati wa kutoka wa kimsingi na kiufundi utakusaidia kuepuka makosa kama vile kufanya biashara kwa hisia na mihemko au kutofunga biashara inayopata hasara. Viashiria muhimu kama vile mistari ya support na resistance ni njia inayotegemea ukweli ya kuelewa mwelekeo wa soko. Taarifa kuhusu mistari ya support na resistance pia inaweza kuangazia upeo wa mabadiliko ya bei ya rasilimali.
Unapoweka biashara, tumia taarifa hii kutambua bei ambazo utafungia biashara zako – ili kuhakikisha faida yako inayowezekana au kudhibiti hasara ikiwa soko litabadilika mwelekeo. Lakini muhimu zaidi, epuka kubadilisha mpango wako ili uweze kushughulikia biashara yoyote kwa lengo thabiti ikiwa haitaenda kama ulivyopanga.
Hatua 3 – Tumia vipengele vya udhibiti wa hatari
Kufanya biashara ni shughuli yenye hatari kubwa, na njia bora ya kukabiliana na hali yenye hatari kubwa ni kuwa na wavu wa usalama hata kama umejiandaa kikamilifu. Wavu huo wa usalama ni kutumia vipengele vya udhibiti wa hatari ili kulinda faida yako inayowezekana na kudhibiti hasara zako wakati soko linapoenda kinyume nawe.
Tuseme wewe ni aina ya mfanyabiashara anayepanua wigo wa uwekezaji wake kwa rasilimali kutoka masoko tofauti. Katika hali hiyo, huenda usiweze kufuatilia mabadiliko ya bei ya rasilimali zote kwa wakati mmoja na kupunguza hasara kwa wakati. Katika hali kama hii, vipengele kama vile Take Profit na Stop Loss vinaweza kukusaidia kulinda faida yako inayowezekana au kupunguza hasara kabla hazijawa kubwa sana, hasa wakati hali ya soko inabadilika kwa kasi.
Hatua 4 – Andika shajara ili kujifunza kuhusu mienendo ya soko la kifedha na mtindo wako wa ufanyaji biashara
Tumia shajara kunakili matukio ya siku yako ya kufanya biashara. Andika ni biashara zipi zilizokuwa na faida na zipi hazikuwa na faida. Ongeza maelezo kwenye kila mojawapo, ukitaja data gani uliyotumia kufanya utabiri wako na maarifa yoyote au mafunzo ya zamani yaliyoathiri mchakato wako wa kufanya maamuzi.
Mbali na kukusaidia kubaki na lengo thabiti, shajara hii itakuwa na manufaa katika kuelewa jinsi masoko yanavyoitikia matukio mbalimbali ya kimataifa na kiuchumi na kugundua wewe ni aina gani ya mfanyabiashara. Kwa muda mrefu, utajifunza kuepuka makosa ya ufanyaji biashara, kuboresha ujuzi wako wa ufanyaji biashara, na kuunda mpango wa biashara unaoendana na mtindo wako wa ufanyaji biashara.
Hatua 4 zilizo hapo juu zinaweza kusaidia wafanyabiashara wanaoanza na wale wazoefu kuboresha ujuzi wao wa ufanyaji biashara kupitia kujifunza mara kwa mara, mazoezi, na nidhamu.
Hata hivyo, ikiwa huna uhakika ni soko gani ufanyie biashara, jinsi ya kutumia vipengele vya udhibiti wa hatari, au unataka kujaribu mkakati wa biashara, fanya mazoezi bila hatari ukitumia akaunti ya demo, ambayo inawekewa fedha za pepe mapema. Jisajili leo ili uweze kujaribu hatua hizi.